October 25, 2014

Tulia

VITA VIZURI (2 Timotheo 4:6-7)

Reuben kigame
Nimevipiga vita vizuri
Mwendo wangu nimeumaliza
Nayo imani nimeilinda
Natarajia kupewa taji na Bwana

Nikitizama nyuma sijuti kaka
Nimejifunza kusahau yaliyopita
Sasa najisukuma kwa yalio mbele
Nikimfuata Yesu Mwokozi wangu

Nimevipiga vita vizuri
Mwendo wangu nimeumaliza
Nayo imani nimeilinda
Natarajia kupewa taji na Bwana

Japo imani yangu imetikiswa
Mimi nimeshikiliwa na Yesu Wangu
Hata wakiniacha rafiki zangu
Siri mimi niko na Imanueli

Nifuateni nifuatavyo Yesu
Yeye ni mwanzo na mwisho wa imani yetu
Msishawishike na ulimwengu upitao
Tuvipige vita vizuri

Nimevipiga vita vizuri
Mwendo wangu nimeumaliza
Nayo imani nimeilinda
Natarajia kupewa taji na Bwana

SAUTI (Zaburi 29)

Ulirekodiwa kwa mara ya kwanza na Julie Kigame katika album yake iitwayo ‘Nitakuabudu’.
Sauti Yake Bwana yapendeza mno
Tamu zidi asali imejaa utukufu
Hutetemesha nchi, gharika, misitu, radi
Imejaa adhama, ayala huwazalisha

Sauti Yake Bwana hutuliza roho yangu
Nikichanganyikiwa Sauti huniongoza
Hekaluni mwa Bwana – Sifa, utukufu
Yeye Mfalme milele, nitaimba sifa Zake.

Hutetemesha nchi, gharika, misitu, radi
Imejaa adhama, ayala huwazalisha
Hekaluni mwa Bwana, sifa, utukufu
Yeye Mfalme milele, nitaimba sifa Zake.

HERI SIKU MOJA (Zaburi 84)

Ewe Mungu wa majeshi
Ninapenda kukaa Nawe
Maskani zako zapendeza,
Nazikondea kwa shauku kubwa

Heri siku moja mbele Zako
Kuliko siku elfu mbali na Wewe
E Bwana, nguvu na msaada wangu
‘Takupenda daima

Moyo na mwili Wangu Bwana
Vyakulilia Mungu Wangu
Heri nikose vyote Baba
lakini nikupate Wewe

Heri siku moja mbele Zako
Kuliko siku elfu mbali na Wewe
E Bwana, nguvu na msaada wangu
‘Takupenda daima

ALPHA NA OMEGA (Ufunuo 1:17)

(Mwandishi asiyejulikana)
We ni Alpha na Omega
Twakuabudu pekee, Wastahili sifa
We ni Alpha na Omega
Twakuabudu pekee, Wastahili sifa

Twakupa utukufu
Twakuabudu Bwana, Wastahili sifa

We ni Alpha na Omega
Twakuabudu pekee, Wastahili sifa
We ni Alpha na Omega
Twakuabudu pekee, Wastahili sifa

Twakupa utukufu
Twakuabudu Bwana, Wastahili sifa

Heshima zote, sifa zote
Heshima zote, sifa zote
Heshima zote, sifa zote
Heshima zote, sifa zo-ooote
Twakuabudu Bwana, Wastahili sifa

IMANUELI (Isaya 9:6-7; Matayo 1:23)

Imanueli Imanueli, Mungu pamoja nasi
Mshauri wa ajabu, Mfalme wa amani
Imanueli, Imanueli

Baba wa milele Yuko nasi
Imanueli! Imanueli!
Sisi si yatima tuko Naye
Imanueli! Imanueli!
Tukidharualiwa, Yuko nasi
Imanueli Imanueli
Na wakati wa huzuni Yuko nasi
Imanueli! Imanueli!

Imanueli! Imanueli!
Mungu pamoja nasi
Mshauri wa ajabu,
Mfalme wa amani
Imanueli! Imanueli!

Tukipitia shida Yuko nasi
Imanueli! Imanueli!
Kwa njaa na magonjwa Yuko nasi
Imanueli! Imanueli!
Wazazi wakikukana Yuko nawe
Imanueli! Imanueli!
Hata ukikosa lishe Yuko nawe
Imanueli! Imanueli!

Imanueli! Imanueli!
Mungu pamoja nasi
Mshauri wa ajabu,
Mfalme wa amani
Imanueli! Imanueli!

Imanueli! Imanueli!

FAIDA TELE (Zaburi 103:2)

Nina faida tele kwasababu Yako Yesu
Dhambi zangu zimeoshwa kwa damu Yako takatifu
Mimi ni mshindi, mriithi wa Ufalme Wako
Nina faida tele kwasababu Yako Bwana

Nimeshinda kifo kwasababu Yako
Kwa kupigwa Kwako uponyaji napata
Shetani ameshindwa hana mamlaka tena
Naimba haleluya, pokea sifa Bwana

Nina faida tele kwasababu Yako Yesu
Dhambi zangu zimeoshwa kwa damu Yako takatifu
Mimi ni mshindi, mriithi wa Ufalme Wako
Nina faida tele kwasababu Yako Bwana

Umeyatuliza maisha yangu
Umenitakasa ni kiumbe kipya
Kama sio Wewe ningekuwa wapi
Nina faida tele maishani mwangu Bwana

Nina faida tele kwasababu Yako Yesu
Dhambi zangu zimeoshwa kwa damu Yako takatifu
Mimi ni mshindi, mriithi wa Ufalme Wako
Nina faida tele kwasababu Yako Bwana

MUNGU MTAKATIFU

David Yared –umerekodiwa kwa idhini ya mtunzi
E Mungu Wangu, Jehovah Baba
Uliniumba nikuabudu
Uhai Wangu, maisha yangu
nakukabithi E Mungu

Jina Lako lina nguvu
Mkono wako watenda makuu
Mimi nitasifu haki Yako
na wema Wako E Baba

Wewe ni Mungu Mtakatifu
Mbingu na nchi zime jawa
Na utukufu Wako
We Ni Mungu Mtakatifu

Kwa uwezo Wako ukaniumba,
‘Kanipa uwezo wa kutawala
Viumbe vyote ulivyoumba
Utukuzwe E Mungu

Mimi Baba ni kitu gani
Unanijali jinsi hii
Ulimtuma Mwana Wako
Akanifia E Baba

Wewe ni Mungu Mtakatifu
Mbingu na nchi zimejawa
Na utukufu Wako
Wewe ni Mungu Mtakatifu

Wewe ni Mungu Mtakatifu
Mbingu na nchi zime jawa na utukufu Wako
Wewe Ni Mungu Mtakatifu

Milele yote nitakusifu
Kwa fadhili Zako Mungu
Sitoacha kulitukuza Jina Lako Ewe Mungu

Wewe ni Mungu Mtakatifu
Mbingu na nchi zimejawa
Na utukufu Wako
We ni Mungu Mtakatifu

I HAVE TASTED/NIMEONJA (Zaburi 34:8; 1 Petro 2:3)

James Kahero- umerekodiwa kwa hiari ya mtunzi
I have tasted of the Lord and I know that Jesus You are good.
I have tasted of the Lord and I know that Jesus You are good.

I know, I know, I know
Yes I know that Jesus You are good
I know, I know, I know
Yes I know that Jesus You are good

Nimeonja Huyu Yesu
Ninajua Yeye ni mwema
Nimeonja Huyu Yesu
Ninajua Yeye ni mwema

Najua-a, Najua!
Ninajua Yeye ni mwema
Najua-a, Najua!
Ninajua Yeye ni mwema

Kisha mpata Huyu Yesu
Utajua Yeye ni mwema
Kisha mpata Huyu Yesu
Utajua Yeye ni mwema

Najua-a, Najua!
Ninajua Yeya ni mwema
Najua-a, Najua!
Ninajua Yeye ni mwema

I know, I know, I know
Yes I know that Jesus You are good
I know, I know, I know
Yes I know that Jesus You are good

WEWE NI BWANA (Yohana 4:23 na 15:13)

Enid Moraa – umerekodiwa kwa idhini ya mtunzi
Wewe ni Bwana, juu ya mabwana
Ufalme wako wadumu milele
Wewe ni Bwana, juu ya mabwana
Umetukuka milele, amina

‘Katoka juu mbinguni
‘Kaja hapa duniani
‘Kamwaga damu kalivari
Ili nipate kombolewa
Nanimeokoka, nimeoshwa dhambi,
Nimekuwa safi, ninakusifu
Milele na milele na milele

Wewe ni Bwana, juu ya mabwana
Ufalme wako wadumu milele
Wewe ni Bwana, juu ya mabwana
Umetukuka milele, amina

Majaribu yaja, shida nazo zaja
Kila siku mbio nikatika vita
Adui hatasita kunimaliza
Nami nimeuona Mkono wa Yesu
Msaada Wangu, Tegemeo Langu, Mwamba Imara, Kwake nasimama
Nimeweka imani kwa Yule Aliye mwaminifu.

Wewe ni Bwana, juu ya mabwana
Ufalme wako wadumu milele
Wewe ni Bwana, juu ya mabwana
Umetukuka milele, amina

TULIA (Kutoka 14:14; 2 Wafalme 6:16)

Tulia kaka, tulia dada
Vita ni Vyake Bwana
Hata dhoruba ivume sana
Vita ni Vyake Bwana

Inua macho yako
Umtazame Mwokozi
Wale walionawe wanaziidi
Majeshi ya adui zako

Tulia, tulia, tulia sasa
Sichukue hatua nyingine
Sikiza sauti ya Mungu wako
Akuwazia mema

Inua macho yako
Umtazame Mwokozi
Wale walionawe wanaziidi
Majeshi ya adui zako

Usiogope, Usitikiswe
Usitazame kando
Weka imani kwa Mungu wako
Vita ni Vyake Bwana leo

Inua macho yako
Umtazame Mwokozi
Wale walionawe wanaziidi
Majeshi ya adui zako

NAOMBA UTULIVU (Yakobo 4:10; Zaburi 23)

James Kahero-umerekodiwa kwa hiari ya mtunzi
Naomba utulivu nikinyenyekea mbele Zako
Siwezi pekee yangu
Kwasababu mimi ni dhaifu
Naomba nguvu Zako x2

Kamwe mimi siwezi!
Mola nipe uwezo

Bwana ni Mchungaji wa maisha yangu
Sitapungukiwa na kitu
Hunilaza penye majani mabiichi
Huniongoza kwa njia za haki
Katika bonde la mauti Yeye Yu nami
Si ajabu Yeye Hunituliza

Naomba utulivu nikinyenyekea mbele Zako
Siwezi pekee yangu
Kwa sababu mimi ni dhaifu
Naomba nguvu Zako x2

Kamwe mimi siwezi
Mola nipe uwezo

Nani anifaaye ila Mwokozi
Mfariji Wangu, rafiki
Nguzo Yangu na Ngome Yangu
Mwamba Wangu aliye imara
Katika bonde la mauti Yeye Yu nami
Si ajabu Yeye Hunituliza

Naomba utulivu nikinyenyekea mbele Zako
Siwezi pekee yangu
Kwa sababu mimi ni dhaifu
Naomba nguvu Zako…

TUTAONANA TENA (1 Wathesalonike 4:13-18, 1 Wacorintho 15: 51-58)

Bwana amuitapo
Mpendwa katika Kristo
Machozi hayaishi kutiririka!
Hakuna maliwazo
Ya kutosha roho zetu
Ila ahadi Yake Bwana wetu

Tutaonana tena, tutaonana tena
Yesu ashukapo mawinguni
Kutunyakua
Msihuzunike kama wasio na tumaini,
Neno latuhakikishia, tutaonana tena

Kufumba na kufumbua
Baragumu iliapo
Tutabadilishwa miili yetu!
Heri walalao katika Kristo Yesu
Kazi na matendo yao
Huwafuata

Tutaonana tena, tutaonana tena
Yesu ashukapo mawinguni
Kutunyakua
Msihuzunike kama wasio na tumaini,
Neno latuhakikishia, tutaonana tena