Amani Moyoni
MAJINA YATAPOITWA
Baragumu yake bwana wakati ikipigwa
Na siku ya milele ikafika
Hapo waliokombolewa watukusanyika
Nitakuwapo jina kuitika.
Majina yatapoitwa
Majina yatapoitwa
Majina yatapoitwa
Nami nitakuwa pamoja nao
Wafu wa Kristo wafufukapo siku ile
Nitashiriki na fahari yake
Waliochaguliwa watakaribishwa kwake
Nitakuwapo jina kuitika.
Chorus
Bwana Yesu atakaporudi toka mbinguni
Siku ya furaha itawadia
Wafuasi wake watakapo kutana huko
Nitakuwapo jina kuitika.
Chorus x3
Nami nitakuwa pamoja nao
Nami nitakuwa pamoja nao
SALAMA INSTRUMENTAL TALK
Hujambo rafiki mpendwa
Mimi ni Reuben Kigame
Naningependa kukuambia kidogo tu
Kuhusu wimbo huu
Wimbo huu uliandikwa na mtu mmoja
Ambaye naambiwa jamii yake yote iliangamia baharini.
Nafikiri hiyo ni ajali ya kushtua sana.
Namimi nashangaa kwa nini yeye baada ya kupoteza jamii yake yote aliweza kuimba wimbo huu na kusema
Ni salama rohoni
Nami nimejifunza mambo mengi sana kutoka kwa huu wimbo.
Ni me jifunza nisi tegemee vitu ama watu ambao wanapita kwa haraka
Nimejifunza kutotegema vitu ambavyo havitanifaidi baada ya kufa.
Na pengine wewe unategemea vitu fulani kama vile pesa, mali, mashamba na vitu vingine ambavyo huwezi kufaidi kwavyo baada ya kufa.
Pesa za weza kuisha. Kazi unaweza kufutwa. Marafiki waweza kukutoraka na kukuwacha. Mashamba yaweza kunyakuliwa. Jee haya yakifanyika itakuwa salama kweli?
Utafaidika vipi?
Naomba kwamba tangia leo uweke tegemeo lako kwake Yesu Kristo ambaye ni Mwamba imara. Hatikiswi. Habadiliki.
Lakini usalama wa hakika ni kwamba dhambi zako zote ziondolewe. Utaweza kuimba ni salama rohoni.
Unaweza kumwita Yesu sasa. Naye atakusamehe dhambi zako zote. Mwambie Bwana, njoo katika maisha yangu nibadilishe. Nipe amani niwe salama rohoni.
Salama rohoni
Ni salama rohoni mwangu
SALAMA ROHONI
Nionapo amani kama shwari
Au nionapo shida
Kwa hali zote
Umenijulisha
Ni salama rohoni mwangu
Ingawa shetani atanitesa
Nita jipa moyo kwani
Kristo ameona unyonge wangu
Amekufa kwa roho yangu
Salama Salama Rohoni rohoni
Ni salama rohoni mwangu x2
Dhambi zangu zote
Wala si nusu
Zimewekwa msalabani
Wala sichukui
Laana yote
Ni salama rohoni mwangu
Chorus
Ni salama rohoni mwangu x2
SI NJIA RAHISI
Si njia rahisi ya kwenda mbinguni
Miiba mingi safarini
Si njia rahisi
Lakini ninaye mwokozi aliyenifia
La, La si njia rahisi
La, La si njia rahisi
Kutembea na Yesu
Huongoza safari
Mazito huya rahisisha
Si njia rahisi
Mashaka ni mengi
Mapigo nayo majaribu
Vikwazo vimo tele
Lakini najua Mwokozi yu pamoja nami
Chorus
Najipa moyo hima
Mwokozi aweza kunishindia haya yote
Tashinda kwa imani amenitangulia Naweza mambo yote kwake
Chorus
Kutembea na Yesu
Huongoza safari
Mazito huya rahisisha
WAKATI WANGU KUOMBA
Wakati wangu kuomba
Umenialika kusali
Nimsihi Mungu Mwenyezi
Anitulize kwa mapenzi
Nyakati za shida nyingi
Ni me pata ufanisi
Na wewe nitangojea
Ewe wakati wa kuomba
Wakati wangu kuomba
Umeniletea furaha
Pamoja nao wenzangu
Nashirikiana na mungu
Mahali hapa nikae
Uso wa Mungu niuone
Na wewe nitangojea
Ewe wakati wakuomba
Wakati wangu kuomba
Mabawa yako hunishika
Kwa Yesu aliye kweli
Aningojea kubariki
Tangu alinialika
Nimwamini kwa hakika
Na wewe nitangojea
Ewe Wakati wa kuomba x3
YESU KWETU NI RAFIKI
Yesu kwetu ni rafiki
Huambiwa haja pia
tukiomba kwa Babaye
maombi asikia
lakini twajikosesha
twajitweka vibaya
kwamba tulimuomba mungu
Dua angesikia
una dhiki na maonjo
una mashaka pia
haifai kufa moyo
Dua atasikia
hakuna mwingine mwema
wakutuhurumia
atujua tu dhaifu
maombi asikia
je hunayo hata nguvu
huwezi kuendelea
ujapodharauliwa
Ujaporushwa pia
watu wangekudharau
wapendao dunia
Hukuambata mikononi
Dua atasikia x3
YESU NAKUPENDA
Yesu nakupenda
Kweli we u wangu
Kwako nazileta
Dhambi zangu zote
Mkombozi wangu
Na mwokozi wangu
Yesu nakupenda
Sasa na daima
Nakupenda kwani
Ulinipenda mbele
Deni ‘kanilipia
Msalabani
Na taji la miiba
Ukavumilia
Yesu na kupenda
Sasa na daima
Milele utukufu
Makaoni mwako
Huko takusujudu
Milele daima
‘Taimba na taji yangu
Ya kumeremeta
Yesu nakupenda
Sasa na daima
Taimba na taji yangu
Ya kumeremeta
Yesu nakupenda
Sasa na daima
Sasa na daima.
AMANI MOYONI
Tangu siku hiyo alipo nijia
Akae moyoni mwangu
Sina giza tena ila mwanga tu
Kwa Yesu mwokozi wangu
Amani moyoni mwangu
Kwa Yesu mwokozi wangu
Sina shaka kamwe
Kwa sababu yeye
yu nami moyoni mwangu
sina haja tena ya kutangatanga
ndiye kiongozi wangu
dhambi zangu zote zimeondolewa
na Yesu mwanawe Mungu
chorus
matumaini yangu ni ya hakika
katika mwokozi wangu
hofu zangu na hamu zimeondoka
kwa kuwa ni naye Yesu
Chorus x2
Yu nami moyoni mwangu x2
BWANA MUNGU NASHANGAA
Bwana Mungu nashangaa kabisa
Nikifikiri jinsi vilivyo
Nyota, ngurumo vitu vyote pia
Vil’o umbwa kwa uwezo wako
Roho yangu na ikuimbie
Jinsi wewe ulivyo mkuu
Roho yangu na ikuimbie
Jinsi wewe ulivyo mkuu
Nikitembea pote duniani
Ndege huimba nawasikia
Milima hupendeza macho sana
Upepo nao nafurahia
Chorus
Kristo arudipo kunichukua
Nitabubujikwa na furaha
‘Tamsujudia mbiguni milele
‘Tatangaza Mungu alivyo mkuu
Chorus x2
Jinsi wewe ulivyo mkuu x2
HUNIONGOZA MWOKOZI
Huniongoza mwokozi
Ndipo nami hufurahi
Niendapo pote napo
Ataniongoza papo
Hun’ongoza hunishika
Kwa mkono wa hakika
Nitaandamana naye
Kristo aniongozaye
Pengine ni mashakani
Nami pengine rahani
Ni radhi ijayo yote
Yuko nami siku zote
Chorus
Mkono akinishika
Kamwe sitanungunika
Atakachoniletea
Ni tayari kupokea
Chorus
Kristo aniongozaye
KAA NAMI
Kaa nami ni usiku tena
Usiniache gizani Bwana
Msaada wako haukomi
Niko peke yangu
Kaa nami
Nina haja nawe kila saa
Sina mwingine wakunifaa
Mimi nitaongozwa na nani
Ila wewe Bwana
Kaa nami
Nilalapo nikuone wewe
Gizani mwote nimulikiwe
Nuru za mbinguni hazikomi
(Siku zangu zote
Kaa nami) x2
KARIBU NA WEWE
Karibu na wewe Mungu wangu
Karibu zaidi Bwana wangu
Siku zote niwe karibu na wewe
Karibu zaidi Mungu wangu
Mimi na safiri duniani
Pakupumzika sipaoni
Nilalapo niwe karibu na wewe
Karibu zaidi Mungu wangu
Na nielekezwe karibu na wewe
Karibu zaidi Mungu wangu
NI WAKO BWANA
Ni wako Bwana
Nimesikia sauti ya mapenzi
Nivute Bwana kwayo imani
Nizidi kusongea
Bwana vuta vuta nije nisonge
Kwako msalabani
Bwana vuta vuta nije nisonge
Kwa damu ya thamani
Nitakase nikutumikie
Kwa nguvu za neema
Roho yangu ikutumaini
Nitende upendavyo
Chorus x2
Kwa damu ya dhamani
MIKONONI MWA YESU
Mikononi mwa Yesu
Kifuani mwake
Pale mapenzi tele
Pumziko moyoni
Sauti za wajumbe
Zaleta habari
Ya utukufu wake
Katika safari
Chorus
Mikononi mwa Yesu
Mashaka hakuna
Kinga majaribuni
Dhambi hazidhuru
Ni huru majonzini
Mashaka na hofu
Majaribu machozi
Ni mda yapita
Chorus
Pumziko moyoni
MWAMBA WENYE IMARA
Mwamba wenye imara
Kwako nitajificha
Hayo maji na damu
Toka mbavuni mwako
Dhambi zangu takasa
Mzigo kuondoa
Sina cha mkononi
Naja msalabani
Ni tupu univike
Nimyonge nishike
Mimi mchafu naja
Nioshe Bwana nisife
Maisha yaishapo
Na mauti yajapo
Nipaapo Mbinguni
Nikuone enzini
(Mwamba wenye imara
Kwako nitajificha) x2
MBELE NINA ENDELEA
Mbele nina endelea
Nina zidi kutembea
Maombi uyasikie
E Bwana unipandishe
E Bwana uniinue
Kwa imani nisimame
Nipande milima yote
E Bwana unipandishe
Nisikae duniani
Mahali pa majaribu
Natazamia Mbinguni
Nitafika kwa imani
Chorus
Nataka nipandishwe juu
Zaidi yale mawingu
Ninaomba nifikishwe
E Bwana unipandishe
Chorus
(Nipande milima yote
E Bwana unipandishe)x2